Ongoza Mabadiliko
Sema 'HAPANA' kwa ndoa za utotoni.
Sema 'NDIYO' kwa maisha ya siku zijazo.
Kila sauti ni Muhimu.
+ 153964
Ahadi zilizotolewa
+ 153964
Ahadi zilizotolewa
Someone pledged 1 minute ago..
Someone pledged 1 hour ago..
KUTANA NA BINTI
Mambo, jina langu ni Binti.
Nina umri wa miaka 14, na ninaishi Tanzania. Napenda kwenda shule, na siku moja natamani kuhitimu elimu ya chuo kikuu. Ndoto yangu ni kuwa mhandisi na kujenga barabara na madaraja katika nchi yangu nzuri na hata nje ya Afrika.
Ndoto yangu itatimia endapo wazazi wangu wakiniruhusu kumaliza shule na kunisaidia kukua na kuwa kila kitu ninachopaswa kuwa.
Bado ndoa za utotoni ni jambo la kawaida sana nchini Tanzania na huharibu ndoto za mabinti wengi sana.Ungana nami katika kuongeza ufahamu na kusaidia mabadiliko katika sheria ili ziwe bora zaidi.
Hii ni kwa kila msichana, kama mimi.
Tuongee tena hivi karibuni,Binti
Kwa nini kampeni hii?
Ndoa za utotoni huwanyima mabinti fursa mbalimbali ikiwemo elimu bora, huduma bora za afya na ulinzi. Inawaweka kwenye umasikini na huwafanya kuwa katika hatari zaidi ya unyanyasaji wa kijinsia, magonjwa ya zinaa n.k. Ndoa za utotoni huongeza hatari ya vifo kwa mama mwenye umri mdogo na mtoto wake pia
Kwanini #TokomezaNdoaZaUtotoni Tanzania?
- Ndoa za utotoni humaliza utoto na kuathiri vibaya haki za elimu, afya na ulinzi kwa watoto.
- Watoto walioolewa kabla ya umri wa miaka 18 wana uwezekano mkubwa wa kuacha shule na kukosa ujuzi wa kupata pesa za kutunza familia zao au kuchangia jamii.
- Mabinti wanaolewa katika umri mdogo wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kufanyiwa ukatili wa nyumbani, kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwa ni pamoja na VVU na UKIMWI.
- Mabinti wanaolewa katika umri mdogo huzaa watoto waliopo kwenye hatari kubwa ya kufariki kutokana na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua.
- Ndoa za utotoni huathiri vibaya uchumi wa Tanzania na kutengeneza njia zaidi za kuelekea kwenye mzunguko wa umaskini kati ya vizazi.
Kwanini Sasa?
- Ndoa za utotoni humaliza utoto na kuathiri vibaya haki za elimu, afya na ulinzi kwa watoto.
- Watoto walioolewa kabla ya umri wa miaka 18 wana uwezekano mkubwa wa kuacha shule na kukosa ujuzi wa kupata pesa za kutunza familia zao au kuchangia jamii.
- Mabinti wanaolewa katika umri mdogo wanakabiliwa na uwezekano mkubwa wa kufanyiwa ukatili wa nyumbani, kuambukizwa magonjwa ya zinaa, ikiwa ni pamoja na VVU na UKIMWI.
- Mabinti wanaolewa katika umri mdogo huzaa watoto waliopo kwenye hatari kubwa ya kufariki kutokana na matatizo wakati wa ujauzito na kujifungua.
Nini cha kufanya?
- Jiunge na kampeni ya kuhamasisha #PINGANDOAZAUTOTONI: Saini ahadi kupitia binti.tz!
- Zungumza na familia yako na marafiki kuweka ahadi ya kutoshiriki ndoa za utotoni na kutia saini ahadi hiyo.
- Jadili suala hili shuleni/kazini/vikundi vyako vya kidini na vya vijana au maeneo mengine maalum mtandaoni na nje ya mtandao.
- Mwambie kiongozi wako wa kimila na kidini au mkuu wa chama au taasisi yako ajiunge na kampeni na kupaza sauti dhidi ya ndoa za utotoni kwa kutumia majukwaa yao wenyewe.
- Ripoti kesi za ndoa za utotoni kwa mamlaka husika zinazopatikana katika jamii yako.
Je, Unajua?
- Tanzania inashika nafasi ya 11 duniani kwa idadi ya ndoa za utotoni?
- 6500 wasichana waliacha shule nchini Tanzania mwaka 2020 pekee kutokana na ujauzito?
- Zaidi ya wasichana 3 kati ya 10 nchini Tanzania waliolewa wakiwa watoto?
- Mahakama Kuu na ya Rufaa zimetoa hukumu kuwa ni kinyume cha sheria kuwaozesha wasichana chini ya umriwa miaka 18 kwenye ndoa?
Mabinti wa Tanzania – Tunawasikia!
Hadithi za ujasiri
Usiruhusu hadithi yangu ijirudie
#SuperDadas wangu 🤩🤩 wako hapa na ujumbe muhimu: "Kama tungeolewa tukiwa watoto, tusingelikua hapa tulipo LEO!!" Wanasimama🙌🏾 Wanazugumza🗣 Je Unasikiliza?? Ni wakati wa #TokomezaNdoaZaUtotoni kwa watoto wakike nchini 🇹🇿 Tembelea www.binti.tz!
Posted by Binti on Friday, July 29, 2022
"Kuna athari mbaya sio tu kwa mtoto wa kike na sio kwa wanawake tu, bali kwa taifa. Watanzania wenzangu, hili ni jukumu la kila mmoja kutekeleza jambo hili, si mtu mmoja tu. Kwa pamoja tutakomesha ndoa za utotoni!" - Askofu Dk.Stanley Hotayi, wa Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Arusha na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Baraza la Kikristo Tanzania Saini ahadi yako leo 👉🏾www.binti.tz 💪🏾
Posted by Binti on Thursday, August 4, 2022
Wapendwa wazazi wetu, Mnadeni kwa kila mtoto wa Kitanzania, bila kujali jinsia. Wasichana wanapaswa kucheza na marafiki zao🤗, kumaliza shule 📚na kujitengenezea jina katika taifa letu🇹🇿 bila hofu ya ndoa za utotoni! Asante sana Pr.Mack Malekana, Askofu mkuu wa Kanisa la Waadventista wa Sabato, kusimama nami! Weka ahadi yako leo kutokomeza ndoa za utotoni 👉🏾www.binti.tz
Posted by Binti on Monday, August 8, 2022
Sikilizeni dada zangu🗣❤️ Wasichana hukosa elimu na nafasi ya kuamua maisha yao ya baadaye pale wanapo olewa mapema! Wewe pia unaweza kukomesha swala la ndoa za utotoni! Saini ahadi yako 👉🏾 www.binti.tz SASA🙌🏾
Posted by Binti on Tuesday, August 9, 2022
Wasichana ni watetezi wa haki zao✊🏾Ila tunahitaji ushirikiano wa kaka zetu pia. Ewe, kaka! Je, unasimama nasi? Onyesha umoja wako kwa kusaini ahadi ya kutokomeza ndoa za utotoni 👉🏾 www.binti.tz Vita ni ya sote pamoja!!! Kaka yangu Emmanuel Cosmas ashaweka ahadi yake! Baado wewe tuu💪🏾 #NilindeKwanza #TokomezaNdoaZaUtotoni #Binti #GirlsNotBrides
Posted by Binti on Thursday, August 18, 2022
Watoto wenzangu OYEEEEE 🤩🤩🤩 Wanafunzi hawa kutoka Mungano Primary wananipa furaha kama yote 🥰 Wasichana wanapaswa kucheza na marafiki zao, kumaliza shule na kujitengenezea jina katika taifa letu bila hofu ya ndoa za utotoni! Weka ahadi yako leo kutokomeza ndoa za utotoni 👉🏾www.binti.tz
Posted by Binti on Thursday, September 8, 2022
Muulize Binti
Ikiwa unapenda kuwasiliana na Binti na mashirika ambayo yanayosaidia kutimiza ndoto yake, tafadhali jaza fomu hii:
Pata Msaada
Je unajaribu kujikinga au kumkinga binti dhidi ya ndoa za utotoni?
Hauko peke yako.
Wasiliana nasi:
Simu ya Msaada kwa Watoto
Polisi
Mashirika ya Kijamii
Washirika
Tunafanya kazi kumjengea kila Binti wa Tanzania Maisha bora, endelevu, na kesho yenye ustawi